Tarehe Iliyotumwa 2023-04-10 08:39:06
Masheha wapatiwa mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala
Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imesema masheha wanajukumu kubwa la kusimamia suala zima la elimu hasa katika ngazi ya maandalizi na msingi ukizingatia madarasa hayo yapo katika mabadiliko makubwa ya mtaala. Kaimu Meneja wa Idara ya Mtaala na Vifaa kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar bi Wanu Ali Makame ameeleza hayo katika mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya unaozingatia ujenzi wa umahiri huko katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Dk Shein Rahaleo. Amesema Iwapo masheha watasimamia ipasavyo suala la elimu katika skuli zilizomo ndani ya shehia zao, mabadiliko ya mtaala yataweza kufikia lengo lake la kuwajenga umahiri wanafunzi kuanzia ngazi ya maandalizi. Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi ya Elimu ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imefanya mabadiliko ya mtaala kwa kuzingatia sera ya elimu ya Zanzibar pamoja na mabadiliko ya sayansi na teknolojia Duniani . Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema licha ya kuwa na mabadiliko ya mtaala lakini ni vyema kukazingatiwa idadi ya wanafunzi ili nia njema ya Serikali ya kuubadilisha mtaala liweze kiwikiwi. Akifunga mafunzo hayo Kwa upande wa Mkoa wa Mjini Magharib Afisa Elimu Mkoa huo nd Mohammed Abdalla mohd amewataka masheha hao kumtumia nafasi zao kuhakikisha jamii inapata uwelewa wa dhana ya mtaala wa umahiri ili uweze kutekelezwa kama malengo ya Serikali yalivyo. Mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya kwa masheha yaliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar yanafanyika katika mikoa yote Unguja na Pemba.
Tarehe Iliyotumwa 2023-03-31 15:50:41
Kuendeleza ushirikiano baina ya TEZ na TET
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUPITIA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR ITAENDELEA KUSHIRISHIKIANA NA TAASISI YA ELIMU TANZANIA KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KITAALUMA ULIOPO. KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO ND KHAMIS ABDALLAH SAID AMEELEZA HAYO ALIPOTEMBELEA OFISI ZA TAASISI YA ELIMU TANZANIA ZILIZOPO JIJINI DAR ES SALAM KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO BAINA YA TAASISI MBILI HIZO. AMESEMA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR AMBAYO IPO CHINI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI INAFANYAKAZI ZINAZOLINGANA ZA UANDAAJI WA MITAALA HIVYO NI VYEMA KUWA NA MASHIRIKIANO YATAKAYOIMARISHA KAZI ZAO. KATIKA HATUA NYENGINE KATIBU MKUU HUYO ALIYEAMBATANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA ELIMU ZANZIBAR WALIPATA NAFASI YA KUTEMBELEA STUDIO ZA KISASA ZA TAASISI YA ELIMU TANZANIA AMBAZO ZINAFANYAKAZI YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI KWA NJIA YA KIELEKRONIKI. KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA ELIMU YA TANZANIA DKT ANETH KOMBA AMESEMA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA TAASISI HIYO NA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR NDIO ULIOSAIDIA KASI ZA MITAALA INAYOANDALIWA KWA SASA KUFANYIKA KWA URAHISI.
Tarehe Iliyotumwa 2023-03-31 15:44:41
Utoaji wa Mafunzo ya Mtaala kwa Walimu Wakuu
WALIMU WAKUU WAMETAKIWA KUWAHIMIZA WALIMU JUU YA UTEKELEZAJI WA MTAALA MPYA KWA MUJIBU WA MAFUNZO WANAYOPATIWA ILI KUFIKIA LENGO LA UTEKELEZAJI MZURI WA MTAALA HUO. KATIBU WA BARAZA LA ELIMU NA MRAJIS WA ELIMU ZANZIBAR BI HAFSA ABOUD TALIB AMEELEZA HAYO ALIPOKUWA AKIFUNGA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA MTAALA MPYA KWA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA SERIKALI NA BINAFSI YALIYOFANYIKA KITUO CHA WALIMU KIEMBESAMAKI. BI HAFSA AMESEMA LENGO LA TAASISI YA ELIMU KUTOA MAFUNZO HAYO KWA WALIMU WOTE NI KUHAKIKISHA MABADILIKO YA MTAALA YANAKWENDA KUTEKELEZWA VIZURI KAMA MALENGO YA SERIKALI YALIVYOPANGWA. AMESEMA KWA SASA WIZARA YA ELIMU KUPITIA TAASISI YA ELIMU INATEKELEZA MTAALA MPYA WA UJENZI WA UMAHIRI KWA NGAZI YA MAANDALIZI MWAKA WA KWANZA, DARASA LA KWANZA, LA NNE NA LA SABA. KWA UPANDE WAO WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO WAMESEMA MABADILIKO YA MTAALA YAMEKUJA KURAHISISHA KAZI YA UFUNDISHAJI KIUTENDAJI AMBAPO ITASAIDIA KUBORESHA ELIMU HASA YA MAANDALIZI NA MSINGI. SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IPO KATIKA MABADILIKO YA MTAALA WA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI NA TAYARI KWA BAADHI YA MADARASA YAMESHAANZA KUTUMIA MTAALA HUO NA KWA MADARASA MENGINE YATAENDELEA KWA UTARATIBU ULIOPANGWA.
Tarehe Iliyotumwa 2023-02-27 15:44:41
Mafunzo ya Upitiaji wa vitabu katika mtaala mpya
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Aneth Komba amewataka walimu wanaofundisha ngazi ya maandalizi na msingi kufuata misingi ya mtaala mpya wa ujenzi wa umahiri ili lengo la Serikali la kuwa na Elimu bora liweze kufikiwa Akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya unaozingatia ujenzi wa umahiri kwa walimu wa darasa la nne huko kituo cha Walimu Dunga wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja amesema hatua hiyo itasaidia kufikia malengo ya kubadilishwa kwa mtaala kutoka ule wa nadharia na kuja wa vitendo. Amesema azma ya Serikali ya kubadisha mtaala huo ni kuona unaendana na mazingira halisi ya Zanzibar hali itakayosaidia wanafunzi watakapomaliza elimu ya msingi kuwa na uelewa . Amesema somo la sanaa za ubunifu na michezo limekwenda kuakisi dhana ya uchumi ambao ndio malengo makuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Mkurugenzi huyo ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kwa hatua iliyofikia ya kuanza kutumia mtaala mpya unaokwenda kuijenga upya Zanzibar kielimu. Mapema Meneja wa Utafiti na Udhibiti Ubora Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd Faridu Muhammed Wakil amesema mtaala wa maandalizi na msingi unaokwenda kutumika kwa baadhi ya madarasa umeakisi malengo ya jamii pamoja na kufanyiwa upembuzi yakinifu. Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kuanzia tarehe 20/2/2023 umeanza kutumia mtaala mpya unaozingatia ujenzi wa umahiri na tayari walimu wa ngazi ya maandalizi mwaka wa kwanza darasa la kwanza tayari wameshapatiwa mafunzo na kwasasa mafunzo yanaendelea kwa darasa la nne.