Tarehe Iliyotumwa 2022-09-28 17:39:35
Utoaji wa mafunzo ya uandishi wa Ramani ya Kitabu (Book map)
Watendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar wametakiwa kuhakikisha wanafuatilia kwa makini Mafunzo wanayopewa juu ya uandishi wa vitabu ili watoto wapate vitabu vyenye ubora.
Ameyasema hayo Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa divisheni ya utayarishaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia Bi Mchanga Ame Saleh ,kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar, wakati akifungua Mafunzo juu ya namna ya utayarishaji wa Ramani ya Kitabu ( book map) kwa Watendaji wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa kituo Cha Elimu Mbadala Raha Leo mjini unguja, amesema Mafunzo hayo ni muhimu sana kwaajili ya kuwa jengea uwezo watendaji wa Tasisi ya Elimu katika utayarishaji wa vitabu vya kiada pamoja na miongozo ya walimu.
Aidha amesema Mafunzo yame kuja wakati muwafaka wakati Taasisi ipo katika hatua ya uandishi wa vitabu vitakavyo tumika katika Mtaala unaotarajiwa kutumika mwakani January 2023.
Amesema kupitia Mafunzo haya watendaji wataweza kuandaa vitabu vya watoto vilivyo Bora vitakavyo saidia kujenga msingi na kuimarisha uwezo wa kusoma, kuhesabu na kuandika .
Aidha ame sisitiza kuwa kutumia fursa hii kwa makini juu ya taaluma inayo tolewa kwaajili ya Taifa letu.
Nae Bwana Masumbuko Ephrahim, Ambae ni mshauri wa kuandaa vitabu vya Elimu kutoka kampuni ya Exford Dar es salaam, amesema lengo ni kuwawezesha watendaji wa Tasisi ya Elimu ya Zanzibar kuweza kuchambua mihutasari na kuandaa mpango wa uandishi wa vitabu vya Maandalizi na Msingi Zanzibar.
Amefahamisha kuwa ili kitabu kiweze kukidhi malengo ya jumla na yale mahususi yalio ainishwa kwenye sera ya Elimu na kwenye mihutasari ya masomo husika ni lazima kuzingatia umahiri na ubunifu ili kipatikane kitabu Bora.
Nao washiriki wa Mafunzo hayo wameishukuru Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kwa kuweza kuwapatia Mafunzo ya namna ya utayarishaji wa vitabu kwaajili ya Taifa letu.