Karibu Taasisi ya Elimu ya Zanzibar

Utoaji wa Mafunzo ya Mtaala kwa Walimu Wakuu


Tarehe Iliyotumwa: 2023-03-31 15:44:41

WALIMU WAKUU WAMETAKIWA KUWAHIMIZA WALIMU JUU YA UTEKELEZAJI WA MTAALA MPYA KWA MUJIBU WA MAFUNZO WANAYOPATIWA ILI KUFIKIA LENGO LA UTEKELEZAJI MZURI WA MTAALA HUO. KATIBU WA BARAZA LA ELIMU NA MRAJIS WA ELIMU ZANZIBAR BI HAFSA ABOUD TALIB AMEELEZA HAYO ALIPOKUWA AKIFUNGA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA MTAALA MPYA KWA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA SERIKALI NA BINAFSI YALIYOFANYIKA KITUO CHA WALIMU KIEMBESAMAKI. BI HAFSA AMESEMA LENGO LA TAASISI YA ELIMU KUTOA MAFUNZO HAYO KWA WALIMU WOTE NI KUHAKIKISHA MABADILIKO YA MTAALA YANAKWENDA KUTEKELEZWA VIZURI KAMA MALENGO YA SERIKALI YALIVYOPANGWA. AMESEMA KWA SASA WIZARA YA ELIMU KUPITIA TAASISI YA ELIMU INATEKELEZA MTAALA MPYA WA UJENZI WA UMAHIRI KWA NGAZI YA MAANDALIZI MWAKA WA KWANZA, DARASA LA KWANZA, LA NNE NA LA SABA. KWA UPANDE WAO WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO WAMESEMA MABADILIKO YA MTAALA YAMEKUJA KURAHISISHA KAZI YA UFUNDISHAJI KIUTENDAJI AMBAPO ITASAIDIA KUBORESHA ELIMU HASA YA MAANDALIZI NA MSINGI. SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IPO KATIKA MABADILIKO YA MTAALA WA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI NA TAYARI KWA BAADHI YA MADARASA YAMESHAANZA KUTUMIA MTAALA HUO NA KWA MADARASA MENGINE YATAENDELEA KWA UTARATIBU ULIOPANGWA.