Karibu Taasisi ya Elimu ya Zanzibar

Kuendeleza ushirikiano baina ya TEZ na TET


Tarehe Iliyotumwa: 2023-03-31 15:50:41

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUPITIA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR ITAENDELEA KUSHIRISHIKIANA NA TAASISI YA ELIMU TANZANIA KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KITAALUMA ULIOPO. KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO ND KHAMIS ABDALLAH SAID AMEELEZA HAYO ALIPOTEMBELEA OFISI ZA TAASISI YA ELIMU TANZANIA ZILIZOPO JIJINI DAR ES SALAM KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO BAINA YA TAASISI MBILI HIZO. AMESEMA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR AMBAYO IPO CHINI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI INAFANYAKAZI ZINAZOLINGANA ZA UANDAAJI WA MITAALA HIVYO NI VYEMA KUWA NA MASHIRIKIANO YATAKAYOIMARISHA KAZI ZAO. KATIKA HATUA NYENGINE KATIBU MKUU HUYO ALIYEAMBATANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA ELIMU ZANZIBAR WALIPATA NAFASI YA KUTEMBELEA STUDIO ZA KISASA ZA TAASISI YA ELIMU TANZANIA AMBAZO ZINAFANYAKAZI YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI KWA NJIA YA KIELEKRONIKI. KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA ELIMU YA TANZANIA DKT ANETH KOMBA AMESEMA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA TAASISI HIYO NA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR NDIO ULIOSAIDIA KASI ZA MITAALA INAYOANDALIWA KWA SASA KUFANYIKA KWA URAHISI.