Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imesema masheha wanajukumu kubwa la kusimamia suala zima la elimu hasa katika ngazi ya maandalizi na msingi ukizingatia madarasa hayo yapo katika mabadiliko makubwa ya mtaala.
Kaimu Meneja wa Idara ya Mtaala na Vifaa kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar bi Wanu Ali Makame ameeleza hayo katika mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya unaozingatia ujenzi wa umahiri huko katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Dk Shein Rahaleo.
Amesema Iwapo masheha watasimamia ipasavyo suala la elimu katika skuli zilizomo ndani ya shehia zao, mabadiliko ya mtaala yataweza kufikia lengo lake la kuwajenga umahiri wanafunzi kuanzia ngazi ya maandalizi.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi ya Elimu ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imefanya mabadiliko ya mtaala kwa kuzingatia sera ya elimu ya Zanzibar pamoja na mabadiliko ya sayansi na teknolojia Duniani .
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema licha ya kuwa na mabadiliko ya mtaala lakini ni vyema kukazingatiwa idadi ya wanafunzi ili nia njema ya Serikali ya kuubadilisha mtaala liweze kiwikiwi.
Akifunga mafunzo hayo Kwa upande wa Mkoa wa Mjini Magharib Afisa Elimu Mkoa huo nd Mohammed Abdalla mohd amewataka masheha hao kumtumia nafasi zao kuhakikisha jamii inapata uwelewa wa dhana ya mtaala wa umahiri ili uweze kutekelezwa kama malengo ya Serikali yalivyo.
Mafunzo ya utekelezaji wa mtaala mpya kwa masheha yaliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar yanafanyika katika mikoa yote Unguja na Pemba.