Ufunguzi wa Mafunzo ya Upimaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd. Abdalla Mohamed Mussa leo Tarehe 16/10/2024 Amefungua mafunzo ya upimaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Maaandalizi na Msingi huko ukumbi wa Ofisi ya Elimu Wilaya ya Mjini Tumekuja. Baadhi ya watekelezaji hao ni pamoja na washauri wa masomo, maafisa mitihani kutoka Baraza la Mitihani Zanzibar, wahadhiri wa vyuo vikuu, wakaguzi wa Elimu, maafisa Takwimu za Elimu wilaya, walimu wa msingi na wakuza Mitaala. Lengo la Mafunzo hayo ni kuwasaidia walimu katika upimaji wa wanafunzi