Kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Abdalla Mohamed Mussa amepokea ujumbe kutoka Taasisi ya Madrasa Early Childhood Programme uliofika Ofisi za Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kufanya kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar, unaofadhiliwa na Shirika la Norwegian Association of Disabled la Norway (NAD). Ujumbe huo umeongozana na wataalamu kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Uganda, Zambia, Norway na Somalia wanaotekeleza mradi wa Elimu Mjumuisho ambapo Lengo la Mkutano huo ni kutambua Mafanikio, changamoto, na kupata mapendekezo ya kuimarisha utekelezaji wa mradi huo.