- Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Viongozi wa Elimu ya Sekondari
- Mafunzo ya Mfumo wa Masjala (e-office)
- Uzinduzi wa programu 10 za Redio za kujifunza lugha ya Kiingereza
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu - Pemba
Pata matukio mapya nahabari mbali mbali kutoka zie.
Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni WEMA Bi, Hafsa Aboud Talib amefunga Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala Mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu huko Skuli ya Pujini Pemba. Mafunzo hayo ya siku tano yametolewa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar ambapo lengo kuu ni kuwajengea uwezo Walimu juu ya kuutekeleza Mtaala mpya kwa mujibu wa hali na mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalumu. Mafunzo hayo pia yametolewa katika Kituo cha Walimu (TC) K/Samaki kwa Unguja.