Kikao kazi cha Kubadilishana Uzoefu katika Masuala ya Elimu ya Watu Wazima
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Abdalla Mohamed Mussa akiwa na Maafisa Taasisi hiyo wamekutana na Uongozi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dar-es-salaaam. Lengo la kukutana Taasisi hizo ni kujifunza kwa kubadilishana Uzoefu katika Masuala ya Elimu ya Watu Wazima na kujenga Uhusiano Mwema baina ya TEZ na TEWW Tanzania Bara. Mkutano huo umeongozwa na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Prof. Michael Ng\'umbi. Mapema Maafisa wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar walifanya ziara katika Vituo mbalimbali vya Elimu ya Watu Wazima ambavyo ni Pamoja na Kituo cha Elimu ya Watu wazima Morogoro (WAMO) kinachofundisha watoto wa kike ambao walipata matatizo mbalimbali na kukaisha masomo, kituo cha CLC Ruvu JKT (MUKEJA) na vituo vya IPOSA-Temeke na Bahati Dar-es-salaam.