Utiaji saini Mkataba wa Uchapishaji Vitabu kwaajili ya Skuli binafsi Zanzibar

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMETILIANA SAINI NA KAMPUNI YA UCHAPISHAJI VITABU YA SEMUKA MKATABA WA UCHAPISHAJI WA VITABU KWA AJILI YA SKULI ZA BINAFSI ZANZIBAR. AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUTIA SAINI MKATABA HUO KATIKA KITUO CHA WALIMU KIEMBESAMAKI, NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI MH. ALI ABDULGULAM HUSSEIN AMESEMA LENGO LA SERIKALI NI KUHAKIKISHA WANANCHI WAKE WANAPATA ELIMU ILIYOBORA HIVYO INACHUKUA JUHUDI MBALIMBALI KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU. AMESEMA SERIKALI IMEKUSUDIA KUWEKA USAWA WA ELIMU KWA SKULI ZOTE ZA SERIKALI NA BINAFSI ILI WANAFUNZI WOTE WAWE NA VIWANGO VYA KUAJIRIKA KIMATAIFA. NAE KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI NDUGU. KHAMIS ABDALLA SAID AMESEMA WAMEONA KUNA MAHITAJI MAKUBWA YA SKULI ZA BINAFSI NA SERIKALI AMEISISITIZA KAMPUNI HIYO KUHAKIKISHA HAWAENDI KINYUME NA MAKUBALIANO YAO YA KUCHAPISHA VITABU HIVYO NDANI YA MIEZI MIWILI KWA VIWANGO VINAVYOHITAJIKA. MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR ND. ABDALLA MOHAMED MUSSA AMESEMA TAYARI WAMEANZA KUTOA VITABU KWA SKULI ZA SERIKALI HIVYO BAADA YA KUKAMILIKA UCHAPAJI WA VITABU VYA SKULI BINAFSI WATAHAKIKISHA VINAWAFIKIA WALENGWA KWA WAKATI. KWA UPANDE WAKE AFISA MASOKO WA KAMPUNI YA SEMUKA WALII HASSAN MIYONGA AMEAHIDI KUWA KAMPUNI YA SEMUKA ITATOA VITABU HIVYO KWA MUDA WALIOKUBALIANA NA KWA UBORA ZAIDI ILI KUSAIDIA UFUNDISHAJI WA WANAFUNZI. AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WALIMU WA SKULI ZA BINAFSI NAIBU KATIBU MTENDAJI JUMUIYA YA SKULI BINAFSI ZANZIBAR (ZAPS) MBAROUK SHAABAN HAJI AMEISHUKURU SERIKALI KWA KUSIKIA KILIO CHAO NA KUAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA PAMOJA ILI KUKUZA SEKTA YA ELIMU NA KUINUA VIWANGO VYA WANANFUNZI.

Huduma Tunazotoa

Huduma zinazotolewa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar.

Mitaala

Kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yanayohusiana na ukuzaji Mitaala ya Elimu ya Maandalizi, Msingi, Elimu ya Sekondari pamoja na Vyuo vya Ualimu

Tafiti

Kufanya tafiti za Elimu na Kuthibiti Ubora kwenye vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Vifaa vya Kufundishia

Kuratibu Utayarishaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia kwa walimu na wanafunzi

Kutoa Mafunzo

Kutoa Mafunzo kazini yanayohusiana na Mitaala na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Viongozi Wetu

23Miaka

Ya uzoefu katika kutoa huduma ya Mitaala

6657Walimu

Jumla ya walimu waliopatiwa
mafunzo ya mitaala

7760Walimu

Tunategemea kuwapatia mafunzo
ya Mtaala mpya 2024

1,222,756
Vitabu vya Mwalimu na Mwanafunzi

Vimeshapishwa kwa ajili
ya mtaala mpya 2024