Mafunzo ya Mtaala mpya kwa walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imeanza kutoa Mafunzo ya Mtaala mpya kwa walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar ili kurahisisha utekelezaji wa mtaala huo ambao unaanza kutumika Rasmi mwezi huu wa January 2025. Akifungua Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd. Abdalla M. Mussa huko katika Kituo cha Walimu Kiembe Samaki Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja amesema Mafunzo hayo yanajumuisha walimu wa skuli za Serikali na Binafsi na yameanza kutolewa kwa walimu wanao fundisha somo la Biashara (business study) ambalo ni somo la lazima kwa wanafunzi wote wa Sekondari na baadae yataendela kwa walimu wa masomo mengine. Aidha amewataka walimu hao kuhakikisha wanayatumia vyema mafunzo hayo ili kwenda kuwajenga vyema wanafunzi. Mafunzo hayo ya Siku tano yanatolewaa na Wataalamu wa somo la Biashara kutoka Taasisi ya Elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Educate na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar.