- Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Viongozi wa Elimu ya Sekondari
- Mafunzo ya Mfumo wa Masjala (e-office)
- Uzinduzi wa programu 10 za Redio za kujifunza lugha ya Kiingereza
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu - Pemba
- Utiaji saini Mkataba wa Uchapishaji Vitabu kwaajili ya Skuli binafsi Zanzibar
- Kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar
- Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu.
- Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu
- Kikao kazi cha Kubadilishana Uzoefu katika Masuala ya Elimu ya Watu Wazima
- Ziara ya Kujenga Uhusiano mwema
- Mjumbe wa Sekretarieti ya GPE Lucinda Ramos ametembelea TEZ
- Mahafali ya Skuli ya High Achievement
- TEZ yapokea Ugeni kutoka Gambia
- TEZ yafanya Mkutano na Walimu wakuu wa Skuli za Sekondari Pemba
- TEZ na TET kuandaa muongozo wa kutolea mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala mpya kwa walimu wa Sekondari.
Pata matukio mapya nahabari mbali mbali kutoka zie.
Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri kwa Wakufunzi ambao wanatarajiwa kuwafundisha walimu wanaofundisha elimu ya msingi (darasa la tatu)
Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imeanza kutoa Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri kwa Wakufunzi ambao wanatarajiwa kuwafundisha walimu wanaofundisha elimu ya msingi (darasa la tatu) hivi karibuni. Mafunzo hayo yameanza tarehe 27/01/2025 katika Kituo cha walimu Michakaini kisiwani Pemba na K/Samaki kwa Unguja. Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri (CBC) awali yalianza kutolewa mwaka 2023 kwa walimu wanaofundisha elimu ngazi ya Maandalizi mwaka wa kwanza, darasa la kwanza, la nne na la saba. Aidha mwaka 2024 mafunzo yaliendelea kutolewa kwa walimu wa Maandalizi mwaka wa pili, darasa la pili na la tano ambapo mwaka 2025 Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa walimu wa darasa la tatu na la sita.