Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri kwa Wakufunzi ambao wanatarajiwa kuwafundisha walimu wanaofundisha elimu ya msingi (darasa la tatu)

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imeanza kutoa Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri kwa Wakufunzi ambao wanatarajiwa kuwafundisha walimu wanaofundisha elimu ya msingi (darasa la tatu) hivi karibuni. Mafunzo hayo yameanza tarehe 27/01/2025 katika Kituo cha walimu Michakaini kisiwani Pemba na K/Samaki kwa Unguja. Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri (CBC) awali yalianza kutolewa mwaka 2023 kwa walimu wanaofundisha elimu ngazi ya Maandalizi mwaka wa kwanza, darasa la kwanza, la nne na la saba. Aidha mwaka 2024 mafunzo yaliendelea kutolewa kwa walimu wa Maandalizi mwaka wa pili, darasa la pili na la tano ambapo mwaka 2025 Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa walimu wa darasa la tatu na la sita.