Mkutano na wadau kukusanya maoni juu ya Mkakati wa Mawasiliano Kuhusu Mtaala wa Umahiri “Curriculum Communication Strategy”.

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar imefanya Mkutano na wadau kukusanya maoni juu ya Mkakati wa Mawasiliano Kuhusu Mtaala wa Umahiri “Curriculum Communication Strategy” ambao umelenga kutoa uelewa kwa jamii. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Elimu wilaya ya Mjini (Tumekuja) na umewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa elimu wa Mikoa, walimu, wanahabari, Vyuo vya ualimu, Maafisa wa WEMA, wastaafu, Wazazi, Kituo cha Habari katika elimu cha Kwarara (KMEC), umoja wa Skuli za binafsi (ZAPS) na asasi za kiraia chini ya Mshauri elekezi kutoka Chuo cha Utawala wa Umma (IPA).