Meneja wa ZIE afungua kikao kazi cha Watendaji Shirika la Room to read.

Meneja Idara ya Mitaala na Vifaa wa Taasisi ya Elimu y aZanzibar Bi, Wanu Ali Makame amefungua kikao kazi cha Watendaji Shirika la Room to read kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Mkoa wa mjini Magharibi. Lengo la Mkutano huo ni kujadili miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni Mradi wa Usawa wa kijinsia na Elimu kwa msichana na mradi wa Usomaji na Maktaba. Kikao hicho kimehushisha washriki kutoka nchi za Afrika na wasimamizi kutoka Marekani.