Mafunzo ya Mtaala wa Umahiri kwa Waajiriwa wapya wa kada ya ualimu wa ngazi ya (Maandalizi na Msingi).

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar inaendelea kutoa Mafunzo ya Mtaala wa Umahiri kwa Waajiriwa wapya wa kada ya ualimu wa ngazi ya (Maandalizi na Msingi). Mafunzo hayo ya siku tano yanaendelea katika Vituo vya walimu Unguja na Pemba ambapo lengo la kutoa Mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu wapya kuufahamu Mtaala wa Umahiri na kuweza kufundishia wanafunzi ili kutoa wanafunzi wenye uwezo wa kujitegemea.