Meneja Idara ya Mitaala na Vifaa wa Taasisi ya Elimu y aZanzibar Bi, Wanu Ali Makame amefungua kikao kazi cha Watendaji Shirika la Room to read kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde Mkoa wa mjini Magharibi. Lengo la Mkutano huo ni kujadili miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni Mradi wa Usawa wa kijinsia na Elimu kwa msichana na mradi wa Usomaji na Maktaba. Kikao hicho kimehushisha washriki kutoka nchi za Afrika na wasimamizi kutoka Marekani.
Taasisi ya Elimu ya Zanzibar ni Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar iliyoanzishwa mwaka 2011 kwa kuzingatia matakwa ya Sera ya Elimu ya mwaka 2006. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeona kuna umuhimu wa kuwa na chombo cha kuratibu na kusimamia mitaala na utafiti wa elimu ili kuimarisha ubora wa elimu hapa Zanzibar. Kwa mujibu wa Sheria Namba 4 ya mwaka 2016 iliyoanzisha Taasisi ya Elimu ya Zanzibar, Taasisi ina mamlaka ya kutayarisha mitaala, vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa skuli za Maandalizi, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu na Elimu isiyorasmi na Watu wazima. Aidha Taasisi inajukumu la kufanya tafiti za kielimu na kutoa mafunzo juu ya utekelezaji wa mitaala.
Kiongozi wa kuandaa mitaala bora na sahihi kutokana na utafiti kwa matumizi ya skuli na vyuo vya ualimu Zanzibar.
Kuongoza utaratibu wa kuandaa mitaala na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia kwa lengo la kuwa na elimu bora na sahihi kupitia utafifiti na ushirikishwaji wa wadau ili kukidhi matakwa ya watu wa Zanzibar
Huduma zinazotolewa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar.
Kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yanayohusiana na ukuzaji Mitaala ya Elimu ya Maandalizi, Msingi, Elimu ya Sekondari pamoja na Vyuo vya Ualimu
Kufanya tafiti za Elimu na Kuthibiti Ubora kwenye vifaa vya kufundishia na kujifunzia
Kuratibu Utayarishaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia kwa walimu na wanafunzi
Kutoa Mafunzo kazini yanayohusiana na Mitaala na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia