Ufungaji wa Warsha ya Siku tano ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa \' Large Scale Assessment\'.

Naibu Katibu Mkuu Taalauma wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir amefunga Warsha ya Siku tano ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa \' Large Scale Assessment\' kwa ajili ya kupima uwezo wa wanafunzi wa darasa la nne na kidato cha pili katika masomo ya Kiswahili, English na Hisabati. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean view Kilimani na imewashirikisha wakuza mitaala kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar na maafisa mitihani kutoka Baraza la Mitihani la Zanzibar chini ya usimamizi wa washauri elekezi kutoka kampuni ya NFER ya nchini Uingereza.