Mahafali ya Skuli ya High Achievement

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Abdalla Mohamed Musaa akiwakabidhi vyeti wanafunzi walio maliza ngazi ya Maandalizi na Msingi katika Mahafali ya Skuli ya High Achievement Iliyopo Mbweni Matrekta. Mahafali hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Verde Mkoa wa Mjini Magharibi. Akizungumza na walimu pamoja na wazazi wa wanafunzi wa skuli hiyo Nd. Abdalla amewapaongeza walimu kwa juhudi kubwa wanazochukua kuwajenga wanafunzi katika malezi Bora. Aidha amewasisitiza kuutumia vyema Mtaala mpya wa Umahiri ambao umekusudia kuwajenga wanafunzi kivitendo. Sambamba na hayo amewataka wazazi wa wanafunzi kufatilia maendeleo ya wanafunzi pamoja na kuwa karibu nao ili kuwalinda na vitendo vya udhalilishaji.