- Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Viongozi wa Elimu ya Sekondari
- Mafunzo ya Mfumo wa Masjala (e-office)
- Uzinduzi wa programu 10 za Redio za kujifunza lugha ya Kiingereza
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu - Pemba
- Utiaji saini Mkataba wa Uchapishaji Vitabu kwaajili ya Skuli binafsi Zanzibar
- Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu.
- Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu
- Kikao kazi cha Kubadilishana Uzoefu katika Masuala ya Elimu ya Watu Wazima
- Ziara ya Kujenga Uhusiano mwema
- Mjumbe wa Sekretarieti ya GPE Lucinda Ramos ametembelea TEZ
- Mahafali ya Skuli ya High Achievement
- TEZ yapokea Ugeni kutoka Gambia
- TEZ yafanya Mkutano na Walimu wakuu wa Skuli za Sekondari Pemba
- TEZ na TET kuandaa muongozo wa kutolea mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala mpya kwa walimu wa Sekondari.
- UDOM na TEZ kukusanya maoni ili kutengeza Moduli mpya za mafunzo ya walimu wa Msingi na Sekondari.
- WEMA Kupokea Ripoti ya upembuzi yakinifu (needs assessement report) ya Upitiaji wa Mitaala ya Mafunzo ya Ualimu.
Pata matukio mapya nahabari mbali mbali kutoka zie.
.jpeg)
Kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Abdalla Mohamed Mussa amepokea ujumbe kutoka Taasisi ya Madrasa Early Childhood Programme uliofika Ofisi za Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kufanya kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar, unaofadhiliwa na Shirika la Norwegian Association of Disabled la Norway (NAD). Ujumbe huo umeongozana na wataalamu kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Uganda, Zambia, Norway na Somalia wanaotekeleza mradi wa Elimu Mjumuisho ambapo Lengo la Mkutano huo ni kutambua Mafanikio, changamoto, na kupata mapendekezo ya kuimarisha utekelezaji wa mradi huo.