- Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Viongozi wa Elimu ya Sekondari
- Mafunzo ya Mfumo wa Masjala (e-office)
- Uzinduzi wa programu 10 za Redio za kujifunza lugha ya Kiingereza
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu
- Muendelezo wa Utoaji wa Mafunzo kwa Walimu - Pemba
- Utiaji saini Mkataba wa Uchapishaji Vitabu kwaajili ya Skuli binafsi Zanzibar
- Kikao cha kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Elimu Mjumuisho Zanzibar
- Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu.
- Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu
- Kikao kazi cha Kubadilishana Uzoefu katika Masuala ya Elimu ya Watu Wazima
- Ziara ya Kujenga Uhusiano mwema
- Mjumbe wa Sekretarieti ya GPE Lucinda Ramos ametembelea TEZ
- Mahafali ya Skuli ya High Achievement
- TEZ yapokea Ugeni kutoka Gambia
- TEZ yafanya Mkutano na Walimu wakuu wa Skuli za Sekondari Pemba
- TEZ na TET kuandaa muongozo wa kutolea mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala mpya kwa walimu wa Sekondari.
- UDOM na TEZ kukusanya maoni ili kutengeza Moduli mpya za mafunzo ya walimu wa Msingi na Sekondari.
- WEMA Kupokea Ripoti ya upembuzi yakinifu (needs assessement report) ya Upitiaji wa Mitaala ya Mafunzo ya Ualimu.
- Mafunzo ya Mtaala mpya kwa walimu wa Skuli za Sekondari Zanzibar
- Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri kwa Wakufunzi.
- Warsha ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa ' Large Scale Assessment'
- Ufungaji wa Warsha ya Siku tano ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa \' Large Scale Assessment\'.
- Mkutano na wadau kukusanya maoni juu ya Mkakati wa Mawasiliano Kuhusu Mtaala wa Umahiri “Curriculum Communication Strategy”.
- Mafunzo ya Mtaala wa Umahiri kwa Waajiriwa wapya wa kada ya ualimu wa ngazi ya (Maandalizi na Msingi).
- Meneja wa ZIE afungua kikao kazi cha Watendaji Shirika la Room to read.
- Kikao baina ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Taasisi ya Goethe Institute ya Ujerumani

Mafunzo ya Mtaala mpya wa Umahiri ngazi ya Sekondari yameanza Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd. Abdalla Mohammed Mussa amewataka walimu kuwatayari kuufanyia kazi Mtaala mpya wa Sekondari ambao unakusudia Kuwawezesha wanafunzi kuwa na ujuzi na utambuzi wa fursa zilizomo kwenye jamii. Akifungua mafunzo ya siku nne kwa wakufunzi wa walimu (TOT) huko katika Kituo cha walimu Michakaini kisiwani Pemba amesema katika utekelezaji wa Mtaala huo ni lazima walimu kuwa na utayari kwani wao ndio watekelezaji wakubwa wa mtaala huo wanaotegemewa katika kuwaandaa wanafunzi darasani. Aidha amewataka Wakufunzi wa walimu wanaopatiwa mafunzo hayo kwenda kuwafahamisha walimu kuwa Mabadiliko ya Mtaala ni jambo la kawaida kulingana na mahitaji ya jamii husika pamoja na Mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Amesema Mafunzo hayo yatawasaidia walimu katika kuutumia Mtaala mpya wa umahiri kwa Ngazi ya Sekondari. Akiwasilisha Mada ya Utelezaji wa Mtaala Ulioboreshwa kwa ngazi ya Sekondari Muwezeshaji Kutoka Taasisisi ya Elimu Tanzania Hwago Hassan Hwago amesema Elimu ya Sekondari sasa itakua na mikondo miwili ambayo ni mikondo wa Jumla na Mkondo wa Amali. Ameeleza kuwa Mtaala mpya wa Sekondari umetoa fursa kwa wanafunzi kujifunza Elimu ya Amali ili kuwawezesha wanafunzi hao kujiajiri wanapomaliza masomo yao.