Mafunzo ya Mtaala mpya kwa Walimu wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu

Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni WEMA Bi, Hafsa Aboud Talib amefunga Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala Mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu huko Skuli ya Pujini Pemba. Mafunzo hayo ya siku tano yametolewa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar ambapo lengo kuu ni kuwajengea uwezo Walimu juu ya kuutekeleza Mtaala mpya kwa mujibu wa hali na mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalumu. Mafunzo hayo pia yametolewa katika Kituo cha Walimu (TC) K/Samaki kwa Unguja.