TEZ na TET kuandaa muongozo wa kutolea mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala mpya kwa walimu wa Sekondari.

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar (TEZ) kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TET) na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali inaendelea kuandaa muongozo wa kutolea mafunzo ya utekelezaji wa Mtaala mpya kwa walimu wa Sekondari. Mafunzo hayo yatatolewa hivi karibuni kwa walimu wote wa skuli za Sekondari za serikali na binafsi. Mtaala mpya wa Sekondari unatarajiwa kuanza kutumika nchini mwezi januari 2025.