Mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu.

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar inaendelea kutoa mafunzo ya Utekelezaji wa Mtaala mpya kwa Walimu wa Maandalizi na Msingi wanaofundisha watoto wenye Mahitaji Maalumu ya kielimu. Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Walimu juu ya kuutekeleza Mtaala mpya kwa mujibu wa mahitaji ya watoto. Mafunzo hayo yanatolewa katika Kituo cha Walimu (TC) K/Samaki kwa Unguja na Michakaini Pemba.