UDOM na TEZ kukusanya maoni ili kutengeza Moduli mpya za mafunzo ya walimu wa Msingi na Sekondari.

Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar (TEZ) wamefanya zoezi la ukusanyaji maoni yatakayo wasaidia katika kutengeneza Moduli mpya za mafunzo ya walimu wa Msingi na Sekondari. Lengo la kukusanya maoni kutoka kwa wadau hao ambao ni pamoja na walimu, wanafunzi, wakaguzi wa elimu washauri wa masomo na wasimamizi wa vituo vya walimu ni kuwawezesha walimu kuutekeleza Mtaala mpya kwa kutumia mbinu shirikishi. Wahadhiri hao wameanza kukusanya maoni kwa upande wa Unguja ambapo siku ya Alhamis tarehe 19/12/2024 wataendelea na zoezi hilo kisiwani Pemba.