Ugawaji wa Vitabu vya Mtaala mpya

Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Inaendelea na zoezi la ugawaji vitabu vya Mtaala mpya na sasa ni Skuli za Wilaya ya Mjini. Vitabu vya Mtaala mpya wa Elimu ngazi ya Maandalizi na Msingi tayari vimeshatolewa kwa skuli mbalimbali za Serikali katika Mkoa wa Kusini na Kaskazini Uguja. Aidha vitabu hivyo pia vitatolewa kwa skuli zote za Serikali Kisiwani Pemba.