Uandaaji wa Muongozo wa watoto wenye Mahitaji Maalumu

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Bi, Salma Haji Saadati amefungua Warsha ya kuandaa Muongozo kwaajili ya Watoto wenye ulemavu wa usikivu na uoni. Warsha hiyo ya siku tatu inaendelea katika ukumbi wa Kituo cha walimu TC K/Samaki. Akifungua warsha hiyo bi, Salma amesema ni jambo jema kuona wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanawekewa nyenzo na mazingira mazuri yanayoendana na mahitaji yao ili nao waweze kupata haki ya Elimu.