WEMA Kupokea Ripoti ya upembuzi yakinifu (needs assessement report) ya Upitiaji wa Mitaala ya Mafunzo ya Ualimu.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imepokea ripoti ya upembuzi yakinifu (needs assessement report) ya Upitiaji wa Mitaala ya Mafunzo ya Ualimu. Ripoti hiyo imewasilishwa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kwa kushirikiana na Washauri Elekezi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania (UDOM, UDSM na SUZA) kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani. Ripoti hiyo itaisaidia Wizara katika utekelezaji wa Mtaala wa Vyuo vya ualimu kwa kuzingatia urejeshwaji wa chuo cha Nkrumah ambapo ubora wa mitaala ni jambo muhimu katika kuimarisha chuo na kupata walimu bora nchini. Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Taaluma Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir ambapo wadau wa Elimu wakiwemo viongozi wa Wizara, Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) na Taasisi mbalimbali za kieleimu walitoa maoni yao ili kuboresha uandaaji wa Mtaala wa Vyuo vya ualimu.